Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAZIRI ULEGA AHIMIZA MAADILI, UWAJIBIKAJI, UFANISI SEKTA YA UJENZI

WAZIRI ULEGA AHIMIZA MAADILI, UWAJIBIKAJI, UFANISI SEKTA YA UJENZI

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma


WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amesisitiza kwamba viongozi wa taasisi za umma wanapaswa kuzingatia maadili ya uongozi, kupiga vita rushwa, kuheshimu utawala wa sheria, na kutunza siri za ofisi.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Ulega amesema kuwa nafasi za uongozi ni dhamana kwa wananchi, si mali binafsi. 


“Ni wajibu wenu kusimamia rasilimali za umma kwa uadilifu na weledi ili kuendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwaletea wananchi maendeleo,” amesema.

Aidha Waziri Ulega amewataka viongozi kuandaa mabaraza ya wafanyakazi katika taasisi zao ili kuimarisha mahusiano kati ya menejimenti na watumishi.

 Amebainisha kuwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi bado yapo, jambo linalohitaji mijadala ya mara kwa mara.

Wizara ya Ujenzi imeelekezwa kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na nidhamu ya kazi Taasisi zote zinapaswa kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.

Ulega ameagiza ripoti za utendaji wa bodi kuwasilishwa miezi mitatu kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha, kisheria.

Viongozi wa taasisi zinazotekeleza mageuzi wanatakiwa kuongeza kasi ya 
 Wakala wa Majengo Tanzania, kwa mfano, umeelekezwa kuandaa mpango wa biashara utakaoiwezesha taasisi hiyo kujiendesha kibiashara.


Aidha ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha miradi ya barabara na viwanja vya ndege inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. 

Aidha, taasisi zinazokusanya maduhuli kama AQRB, ERB, na CRB ziongeze makusanyo na kudhibiti matumizi ili kuimarisha ufanisi na tija.

Waziri Ulega pia amewataka watumishi wa sekta ya ujenzi kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kuepuka rushwa pamoja na matumizi mabaya ya ofisi ili kutoa huduma bora kwa wananchi.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3