Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANAWAKE IRINGA WAELEZA SABABU ZA UKATILI WA KIJINSIA

WANAWAKE IRINGA WAELEZA SABABU ZA UKATILI WA KIJINSIA

  


NA EASTER KAMETA (UoI)

MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA 

Baadhi ya wanawake mkoani Iringa wameeleza sababu  tafauti tofauti za ukatili zinazo wakumba mwanawake katika jamii

Akizungumza na Matukio Daima Paulina Damas mwanamke huyo ameleza kuwa mila na destuli potofu zinapelekea kutokuwepo kwa usawa katika jamii pia na hata kupelekea ukatili dhidi ya wanawake.

"Baadhi ya tamaduni humchukulia mwanamke kama mtu wa daraja la chini au mali ya mwanaume, jambo linalochochea udhalilishaji na ukatili pia Kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia Pale ambapo wanaume hupewa mamlaka makubwa kuliko wanawake katika maamuzi ya kifamilia au kijamii"

Kwa upande wake Warioba Lyana   ameeleza kua matumizi mabaya ya pombe na madawa ya kulevya yana pelekea ukatili kwa mwanamke na kutaja baabhi ya mambo kama kupelekea kupigwa kwa wanawake na pia kuathilika kisaikolojia.

"Matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya  huathiri uwezo wa mtu kufikiri na kudhibiti hasira zake   pia kuleta migogoro katika familia ambapo inaweza kupelekea kupigwa kwa mwanamke na mumewe hali hii inanaweza kusababisha msongo wa mawazo na kuathilika kisaikolojia kwa mwanamke ."

Naye Elizabeth Msigwa  ameeleza baadhi ya sababu kuwa ukosefu wa elimu kuwa hupelekea ukatili , wanaume kutokuwa na uelewa haki za wanawake pia wivu kwa baadhi ya wanaume hupelekea kuwepo kwa ukatili kwa wenza wao.

"Ukosefu wa elimu na uelewa wa haki za binadamu kwa watu wasiojua haki za wanawake wanaweza kuendeleza ukatili bila kutambua kuwa ni kosa la kisheria na kijamii pia Wivu uliopitiliza na ukosefu wa kujiamini Baadhi ya watu hutumia ukatili kama njia ya kudhibiti au kuonyesha umiliki kwa mwenza wao."

Pia Tunu Ezeliel amezungumza juu ya malezi yanayoweza kupelekea mtoto kuwa katili kutokana na maisha aliyo yaishi toka akiwa mdogo alikuwa  anapitia mazingira gani  hivyo hupelekea naye kujua kua ukatili  ndio aina ya maisha.

"Malezi yenye ukatili yanaweza kumfanya mtu aliyekulia katika mazingira hayo  kuweza  kuona ukatili kama jambo la kawaida na kuendeleza tabia hiyo kutokana kwamba ameshazoea kuishi katika mazingira yenye ukatili."

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3