WAISLAM KIGOMA WAOMBWA KUOMBEA AMANI YA DUNIA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Shekhe waMkoa Kigoma Hassan Kiburwa amewaongiza Waumini wa Kiislam mkoani Kigoma katika sala ya Eid huku akihimiza waislam nchini kuombea amani ya dunia.
Shekhe huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa Vita vinavyoendelea duniani ikiwemo ya Iran, Israel na Marekani ina athiri kubwa kwa ulimwengu wote hivyo kuwataka waombe ili vita viishe na amani ya dunia irejee.
Aidha Shekhe Kiburwa amewataka Waislam na wasio waislam kuvumiliana, kudumisha amani na kutendeana yaliyomema
Akiongoza ibada ya Sala Eid iliyofanyika Msikiti Mujahidina Ujiji mkoani Kigoma Shekhe Kiburwa alisema kuwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani iwe mawaidha na darasa la kuwafanya watu wote kufanya mambo mema na kuacha mambo yanayowachukiza wengine.
Shekhe Kiburwa alisema kuwa Amani ya nchi ni jambo muhimu hivyo tofauti zilizopo baina ya waislam katika taratibu za kufunga mwezi wa Ramadhani na kutangaza kuonekana kwa mwezi kumaliza mfungo wa Ramadhani isiwe sababu ya kuwafanya waislam wakafarakana na kuchukiana.
Awali Mwenyekiti wa Taifa wa Taasisi ya Istiqama Foundation, Shekhe Mustafa Khalfani Kiumbe aliwataka waumini wa kiislam kushikana, kupendana na kudumisha umoja wao kwa mawaidha ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo waislam na wasio wa waislam walishikamana na kutendeana mema.
Naye Faqihu Mkuu wa Taasisi ya Isuwat, sheikh Dabas khalfani Kiumbe alisema kuwa wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani watu wote waislam na wasio wa waislam waliungana na kufanya matendo mema kwa kudumisha Amani na usalama nchini na kwamba baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani tabia na matendo hayo yanapaswa kuendelea ili kuifanya nchi yetu kuwa na Amani na salama.
Viongozi hao kwa nyakati tofauti wamewomba waumini wa kiislam kuomba sana kwa Mwenzi Mungu ili dua na sala zao ziweze kusaidia katika kumaliza vita Mashariki ya kati baina ya Iran, Israel na Marekani ambapo mamia ya watu wanauawa na kuharibu uchumi wa dunia na kuvuruga mipangilio ya maisha ya binadamu.



