Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WADAU WA MAZIWA NCHINI KUKAGULIWA NA KUSAJILI NA SERIKALI

WADAU WA MAZIWA NCHINI KUKAGULIWA NA KUSAJILI NA SERIKALI

  

Na Lilian Kasenene Morogoro

Matukio Daima Media

SERIKALI imezindua mpango wa kuwakagua na kuwasajili wadau  wa maziwa nchinii ili watambulike na zao la maziwa lichangie katika pato la taifa 


Msajili wa bodi ya maziwa Tanzania (TDB)Profesa George Msalya alisema maziwa ni biashara  hivyo sekta hiyo inahitaji kuwekwa kwenye mnyororo wa thamani ili maziwa nayo yawe zao na kimkakati.


"Maziwa ni biashara na maziwa ni uchumi...kwa mwaka kaya zaidi ya milioni 4.6 zinanufaika na ajira maziwa yanapokuwa kwenye mnyororo wa thamani,"alisema Profesa Msalya 


Akifungua semina ya maafisa mifugo wa mikoa, msajili huyo alisema kwa sasa sekta ya maziwa inachangia asilimia mbili ya pato la taifa kwa mwaka ila likiwekwa katika mpango wa zao la kimkakati linaweza kuchangia hadi asilimia  2.3

"Ukiacha maziwa kuwa biashara pia ni lishe na chakula muhimu kisicho na madhara kwa mtu yeyote na kinatumika kwa watu wa rika zote," alisema Profesa  Msalya.

Afisa mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mariam Kingu alisema zoezi la usajili pamoja na kuwa ni takwa la kisheria pia ni kwa ajili ya kuwatambua wadau wa maziwa ili nao waweze kunufaika na Fulsa zinazotolewa na serikali.

"Wadau wasiwaogope wakaguzi,  lengo la ukaguzi ni kwa ajili ya kufanya usajili ili wadau wa maziwa nao wanufaike katika mnyororo wa thamani wa ufugaji" alisema Bi Kingu.


Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3