UJENZI FORODHA YA PAMOJA KIGOMA KUGHARIMU BILIONI 47
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (wa pili kulia) akitembelea na kukagua kituo cha forodha cha pamoja (OSBP) kinachojengwa katika eneo la Manyovu kijiji cha Mnanila wilayaa ya Buhigwe mkoani Kigoma mpakani mwa Tanzania na Burundi
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Kiasi cha shilingi Bilioni 47 kinatarajia kutumika kwa utekekezaji wa mradi wa forodha ya pamoja eneo la Manyovu wilaya Bujigwe mkoani huku Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akiitaka Wakala wa barabara nchini (TANROADS) kusimamia na kuzipatia ufumbuzi changamoto zote zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi huo
Akitembelea na kukagua mradi huo Balozi Sirro alisema kuwa changamoto zilizojitokeza zisipopatiwa ufumbuzi haraka zinaweza kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo.
Awali Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Gelawdiwos Tadesse kutoka Kampuni ya Beza Consulting Engineers in Association with G-PES alimwambia Mkuu wa mkoa Kigoma kwamba kushindwa kuondolewa kwa miundo mbinu ya nguzo za TANESCO na malipo ya fidia ya nyumba 15 zilizojitokeza kwenye mzunguko wa Manyovu kijiji cha Mnanila kunaweza kuchelewesha mradi huo.
Akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi huo Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa Kigoma, Mhandisi Chora Kimata alisema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 47 zilitolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kinatarajia kutumika kwa utekelezaji wa mradi huo na tayari Mkandarasi ameshalipwa shilingi bilioni sita na utekelezaji wa mradi umefika asilimia 34.
Akizungumzia changamoto zilizojitokeza alisema kuwa wamekubaliana kumpa Mkandarasi nafasi ya kufanya malipo ya kuhamisha nguzo hizo wakati fedha ya utekelezaji wa jambo hilo ikifanyiwa mchakato huku akibainisha kuwa tayari uthamini wa nyumba hizo 15 na anasubiriwa mtendaji Mkuu TANROADS atoe fedha malipo yaweze kufanyika.
Meneja huyo wa TANRODS mkoa Kigoma alisema kuwa mkataba wa mradi unaonyesha kuwa mradi unapaswa kuanza Julai 25 mwaka 2025 na kukamilika Mwezi Julai 2026 ambapo mkandarasi tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi bilioni sita kama malipo ya awali.


