Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
BILIONI 2.6 KUKAMILISHA  KITUO CHA AFYA MAKERE

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shilingi Bilioni 2.6 zinatarajia kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Makere katika kijiji cha Makere wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo kukamilika kwa kituo hicho kutaondoa adha kwa wananchi wa kata hiyo kutegemea huduma za matibabu kutoka kambi ya wakimbizi ya  Nyarugusu iliyopo wilayani humo.

Meneja wa Wakala wa barabara mkoa Kigoma, Mhandisi Chora Kimata alisema kuwa mradi huo ni sehemu ya miradi 12 ya nyongeza inayotokana na mradi mkubwa wa barabara ya Kiwango cha lami ya Manyovu wilaya ya Buhigwe hadi Kabingo wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Akizungumzia kutekelezwa kwa mradi huo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kasulu, Samuel Kadogo alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya Makere ambao awali msaada mkubwa wa matibabu ilikuwa kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu aambako ilibidi kuingia kwa vibali.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya mipango ya serikali kusogeza huduma kwa wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3