Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!

 

MKUU wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka  amesisitiza  kuzingatiwa kwa maadili katika Jamii Hasa katika kipindi hiki Cha mfungo mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma ili kuipata Jamii iliyo bora.

‎Wakati wa   Iftar iliyoandaliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  Takukuru mkoa wa Njombe Mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda kwa niaba ya mkuu wa mkoa amewataka wananchi na waislamu wote kushirikiana na Taasisi hiyo kukabiliana na vitendo vinavyosababisha mmomonyoko wa maadili kwani hata rushwa inatokana na kukosekana kwa misingi ya maadili.

Awali Shekhe wa mkoa wa Njombe Rajab Msigwa amesema kizazi Bora ni kile kinachopinga rushwa na kutenda haki hivyo kila Mmoja anapaswa kutekeleza wajibu wake. 

‎Kwa upande wake Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Cassim Ephrem amewakumbusha wananchi kuwa jukumu la Kupinga rushwa ni la kila Mmoja hivyo wanaomba ushirikiano kwani na wao ni miongoni mwa Jamii ya Njombe

‎Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo na Halima Abdalah Hamza na George Sanga wamekiri kushirikiana na Takukuru katika mapambano dhidi ya Rushwa  huku wakiwataka Waliopo mamlakani kuyatumia vizuri madaraka Yao. 

‎Waislamu duniani kote wanasubiri mwandamo wa mwezi ili kuhitimisha funga Yao ya siku 30 za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3