JAMII YAASWA KUJENGA UTARATIBU WA KUANDIKA WOASIA MAPEMA NA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA WAKATI WA KUANDIKA WOSIA ILI UWE HALALI
Anold Deogratias Matukio Daima Media
Wananchi wilayani Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kuandika mapema wosia na kufuata njia za kisheria wakati wa kuandika wosia huo ili uwe halali na kuhakikisha wahusika wanapata stahaki zao endapo muhusika atapoteza maisha.
Ushauri huo umetolewa na mwanasheria wa manispaa ya Bukoba Farida Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kliniki ya kupokea na kusikiliza kero za wananchi mjini Bukoba mwanasheria huyo ameeleza kuwa wosia unatakiwa kufuata sheria na taratibu ili uwe halali.
“kuna taratibu maalumu za kuandika na kuacha wosia, kuna ofisi ambazo zinashughulika hayo mambo wananchi wanatakiwa waelewe kwamba wakati wanataka kuandika wosia basi wafuate utaratibuu wa kisheria ili wosia weke uwe wa kisheria na baadae usije ukabatilishwa kwa sababu wosia nyingi zinaonekana hazijafuata taratibu za kisheria”
Aidha mwanasheria huyo amewataka wasimamizi wa mirathi wanaoaminiwa na familia kukusanya mali za marehemu, kuzigawa kwa walengwa na kisha kufunga mirathi kwa wakati ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara ya urithi inayojitokeza katika familia.
“unachotakiwa we msimamizi wa mirathi ukishapokea mirathi hiyo uwagawie warithi na wamiliki mali hizo kwa majina yao, yale majina yahame kutoka kwenye majina ya marehemu na Kwenda kwa mrithi, lakini pia lazima mirathi ifike tamati kwasababu msamamizi wa mirathi anaweza akafa kabla hajamaliza kuwa mirathi hivyo kuleta migogoro katika familia”.
Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Bukoba akiwemo Christina James amesema kuwa sabubu kubwa inayopelekea kuwepo kwa migogoro mingi ya mirathi kwenye jamii ni kutokana upungufu wa elimu ya mirathi kwa wananchi na pia woga kwa wananchi wakiambiwa kufuata sheria ikiwemo kwenda mahakamani”
“hapa kubwa ninaloliona kwa wananchi elimu hawana juu ya mirathi na wananchi waliowengi ni waoga anaamini suala la mirathi mara nenda mahakamani unajua mwingine hata kufika polisi hajawai sasa ukimwambia nenda mahakamani anona hii hapana”
Naye diwani wa kata ya Bilele Tawfiq Sharifu ameitaka serikali kushika chini mpaka kwa wananchi ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya mirathi ili kuepukana ma makosa yanayojitokeza wakati wa kuandaa wosia na pia uteuzi wa wasimamizi wa mirathi.
“sasa serikali ishuke kwa wananchi waende kutoa elimu kwa wananchi kwa sababu imeonekana kundi kubwa la wananchi hawajui masuala ya mirathi lakini pia ni waoga hata kuulizac mambo mengi wanataka wayamalizie kwenye ukoo amaekuja babu au bibi wanaheshimu kauli ya mkubwa hata kama amepindisha mambo”
Kliniki hiyo maalum iliyoanzishwa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Yohana Siima iliyodumu kwa siku nne ilikuwa na lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo wataalamu na maafisa wamewatatulia kero wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Kaitaba.
MWISHO.



