Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MAWASILIANO MIKUMI–IFAKARA YAKWAMA KWA MARA NYINGINE NDANI YA WIKI MOJA, NI BAADA YA DARAJA RUHEMBE KUHARIBIKA...

MAWASILIANO MIKUMI–IFAKARA YAKWAMA KWA MARA NYINGINE NDANI YA WIKI MOJA, NI BAADA YA DARAJA RUHEMBE KUHARIBIKA...

Na Matukio Daima Media, Morogoro 

HUDUMA za usafiri katika barabara inayounganisha Mikumi na maeneo ya Ruaha- Ifakara-Mlimba-Ulanga na Malinyi katika wilaya za Kilosa Kilombero,Ulanga na Malinyi zimeathirika kwa mara nyingine kutokana na uharibifu wa daraja la Ruhembe wilayani Kilosa mkoani Morogoro 

Kukatika kwa Kingo za daraja hilo kumetokea Majira ya Usiku wa kuamkia Machi 13 mwaka huu, ikiwa ni siku chache baada ya daraja jingine katika njia hiyo kuathiriwa Kingo zake usiku wa kuamkia Machi 09 na kushindwa kupitika 

Daraja hilo linaripotiwa kuharibika usiku baada ya kingo zake kusombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kufanya magari kushindwa kupita katika eneo hilo.


Awali akikagua uharibifu wa daraja la awali lililopo Kijiji Cha Mhenda katika barabara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima aliagiza hatua za dharura kuchukuliwa kwa kuweka kivuko cha muda Cha waenda kwa miguu na kueneelea na matengenezo ya haraka ya daraja la kudumu ili vyombo vya moto vipite ambapo wakala wa Barabara TANROADS waliahidi kushughulikia kwa haraka.

Lakini wakati matumaini yakionekana kuanza kurejea na njia kuanza kupitika kwa magari, athari ya daraja la Ruhembe imerudisha nyuma matumaini ya Wananchi katika mawasiliano ya barabara kwa kushindwa kuvuka Tena upande mmoja kwenda mwingine.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3