Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANANCHI WATAKA KITUO CHA AFYA KANDAGA KIKAMILIKE

WANANCHI WATAKA KITUO CHA AFYA KANDAGA KIKAMILIKE

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mabalozi na wanachi wa kata ya Kandaga halmashauri ya wilaya Uvinza mkoani Kigoma wameiomba serikali kukamilisha mradi wa kituo cha afya katika kata hiyo  ili waondokane na adha ya muda mrefu ya kufuata matibabu mbali mrefu na kwa gharama kubwa


Wananchi hao wamesema hayo mbele ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Abdulkadri Mushi wakati wa maadhimisho ya kiwilaya ya sherehe za miaka 49 ya kuzaliwa CCM yaliyoenda sambamba na ukaguzi wa miradi uliofanywa na kamati ya siasa ya mkoa Kigoma.


Mmoja wa mabalozi aliyehudhuria maadhimisho hayo yaliyoenda sambamba na kujitolea kufanya kazi katika mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya, Marystela Kishanga alisema kuwa serikali imetoa fedha na kuahidi mradi huo kuanza kutoa huduma mwezi April mwaka huu hivyo wameomba ahadi hiyo ya serikali itekelezwe.


Akizungumza baada ya kutembelea, kukagua na kushiriki kwenye kazi ya ujenzi wa kituo hicho cha afya Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Abdulkadri Mushi alisema kuwa mradi huo haukuja kws bahati mbaya bali ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambapo ameagiza Mkuu wa wilaya Uvinza na Mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanasimamia na mradi ukamilike kwa wakati.

Awali Msimamizi wa mradi huo Hamisi Mtegeka alisema kuwa wamepokea shilingi milioni 250 kwa ajili ya mradi na tayari shilingi milioni 118 zimetumika na mradi umefika asilimia 50 ukitarajia kukamilika mwezi Machi mwaka huu.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3