KAMANDA WA POLISI IRINGA AHITIMISHA UKAGUZI WA KIUTENDAJI MUFINDI
Feb 5, 2026
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, Februari 4, 2026 amehitimisha ukaguzi wa kiutendaji katika Wilaya ya Mufindi kwa mujibu wa (PGO) namba 47, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utendaji kazi ndani ya Jeshi la Polisi.
Lengo la ukaguzi huo ni kubaini changamoto zinazowakabili askari katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuweka mikakati ya kuboresha zaidi utendaji na ufanisi kazini.
Kamanda Bukumbi alipata fursa ya kukagua Paredi maalum lililoandaliwa kwa heshima yake na kisha kuzungumza na askari wa vyeo mbalimbali ambapo alisisitiza nidhamu, uwajibikaji na kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa manufaa ya jamii.
.jpeg)


.jpeg)

