Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WADAU WA MAENDELEO KAGERA WAOMBA SERIKALI KUONGEZA BAJETI YA BARABARA

WADAU WA MAENDELEO KAGERA WAOMBA SERIKALI KUONGEZA BAJETI YA BARABARA

 


Na Anold Deogratias Matukio Media Kagera

Wadau wa maendeleo mkoa wa mkoa wa Kagera wameiomba serikali kupitia wizara ya ujenzi kuongeza kiwango cha fedha ya utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja mkoani humo ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji na kukuza wa mwananchi mmoja mmoja na wa mkoa kwa ujumla.


Hayo yamejili katika  kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Kagera ambapo moja ya changamoto kubwa iliyowasilishwa katika kikao hicho ni ufinyu wa bajeti ya barabara hali inayokwamisha utekelezaji wa ujenzi wa barabara nyingi na madaraja muhimu mkoani Kagera.

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini mhe.Jonston Mutasingwa amesema ukiangalia kila bajeti kuna kiwango cha fedha kinatumika kulipa madeni ya nyuma hivyo tusipo angalia hata bajeti unaweza kukuta kiwango kikubwa cha fedha kinatumika kulipa madeni ya nyuma, hivyo tuombe serikali iongeze bajeti ya barabara ili miradi ya barabara iwezze kutekelezwa


Naye Mbunge wa Mulaba Kaskazini Adones Bitegeko amesema pamoja na bajeti ya barabara kutengwa ila bado tumeona changamoto kubwa hapa ni kupata fedha ya utekelezaji wa miradi ya fedha kwahiyo tuna haja ya mkoa kusukuma jambo hili kuhakikisha tunapata fedha zaidi.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja mkoa wa Kagera meneja wa wakala wa barabara Tanzania TANROADS  mkoa wa Kagera mhandisi Samweli Mwambungu amesema kuwa changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ni ufinyu wa bajeti unaopeleekea kushindwa kutekeleza miradi mingi.


tuna bilioni kumi na nne   ila uhitaji stahiki ni bilioni 25 ili kutekeleza miradi ya barabara zetu, ufinyu wa bajeti ndio kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yetu, lakini pia changamoto ya mvua imekuwa kikwazo kikubwa kwetu katika ujenzi wa barabara na madaraja.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido ametaka usimamizi mathubuti wa rasmali fedha katika kutekeleza miradi hiyo ili itoe thamani halisi ya fedha.

nisisitize kupitia kikao hiki kuwa utekelezaji wa miradi ya yote ya ujenzi na ukarabati wa barabara tunapaswa kuzingatia usimamizi Madhubuti wa rasimali fedha kila thamani ya fedha lazima ionekane lakini tuzingatie ubora wa barabara zetu

Katika mwaka wa fedha 2026/2027 mkoa wa Kagera umeomba kuidhinishiwa shilingi bilioni 14.5 kwa ajili ya utekelezaji wa  kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara na madaraja, huku uhitaji ukiwa ni shilingi bilioni 25.8 wakiwa na upungufu wa shilingi bilioni 11.3.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3