MBUNGE SIGRADA ATISHIA KUONGOZA MAANDAMANO CHAI KIBENA NJOMBE
Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha ukombozi wa Umma Chauma mkoa wa Njombe Sigrada Mligo ametishia kuongoza maandamano makubwa ikiwemo kufunga barabara kuu ya Njombe Songea baada ya wiki Moja endapo hatma ya madai ya wafanyakazi wa Kiwanda Cha chai Kibena haitapatikana.
Sigrada ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea Kiwanda hicho na kukutana wafanyakazi pamoja na uongozi ulioahidi kutoa majibu baada ya wiki Moja ya lini Malipo ya wafanyakazi hao ikiwemo mishahara ya Mameneja na michango ya NSSF italipwa.
Awali Sophia Mwiter Ofisa rasilimali watu wa kampuni ya DL Group katika Kiwanda Cha Kibena ameahidi kutolea majibu hapo tarehe 2 Machi siku ya Juma Tatu ijayo ya lini watalipa fedha hizo ambazo zimesababisha migomo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi na kwani wapo kwenye mahesabu ya nini anastahili kila Mtumishi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda hicho akiwemo Frida Kidenya Mwenyekiti wa Chama Cha wafanyakazi wa mashambani wanasema wafanyakazi wa chini wanadai michango Yao ya Mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF huku Mameneja wakidai mishahara ya miezi zaidi ya kumi.
Kutokana na Hali hiyo Mbunge wa viti maalumu Chauma mkoa wa Njombe Sigrada Mligo amewataka wafanyakazi hao kuvuta subira katika kipindi hicho Cha wiki Moja baada ya hapo utekelezaji usipofanyika ataongoza maandamano pamoja na kufunga barabara magari yasipite mpaka haki ya wafanyakazi itakapopatikana.
Hata hivyo Wafanyakazi hao wamegoma kuendelea na kazi mpaka watakapolipwa fedha zao zinazotajwa kufikia takribani bilioni Tatu Tangu malimbikizo yaanze.




