TIMU YA WATAALAM LUSHOTO YAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA BUMBULI, SAME IKIWA NI UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU
Feb 27, 2026
Na Ashrack Miraji Matukio Daima
TIMU ya Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, imefanya ziara ya kujifunza na kupata uzoefu kuhusiana na uchimbaji wa madini ya Bauxite Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli na Halmashauri ya Wilaya ya Same.
Ziara hii inakuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alipofanya ziara Wilayani Lushoto 16 Februari, 2026 - 18 Februari, 2026 na kuagiza kampuni ya Abanyambo Enterprises & General Supplies Ltd zenye leseni nne za uchimbaji madini hayo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ziruhusiwe kuanza kufanya uchimbaji.
Ili kutekeleza maelekezo hayo, timu ya Wataalam imetembelea Halmashauri hizo mbili kujifunza na kupata uzoefu jinsi ambavyo zimekuwa zikiratibu shughuli hizo za uchimbaji Katika maeneo yao ambayo kwa kiasi kikubwa sehemu madini hayo yanachimbwa zinafanana Kijografia na Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.
Wakati akisalimia Wananchi wa Lushoto Katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto tarehe 17/02/2026, Mhe. Dkt. Mwigulu, aliagiza Mwekezaji wa kampuni ya Abanyambo Enterprises & General Supplies Ltd mwenye leseni nne za uchimbaji Katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto aruhusiwe kuendelea na uchimbaji.



