Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
ASKARI 758 WAMALIZA MAFUNZO KIDATU, WAKUMBUSHWA UADILIFU

ASKARI 758 WAMALIZA MAFUNZO KIDATU, WAKUMBUSHWA UADILIFU

 

Matukio Daima, Morogoro


Askari 758 wa Jeshi la Polisi wamehitimu mafunzo ya uongozi mdogo katika Chuo cha Polisi Kidatu, wakikumbushwa kuzingatia maadili, uadilifu na uwajibikaji katika utumishi wao.


Kamishna wa Polisi Zanzibar, Kombo Khamis Kombo, alisema mafunzo hayo yamelenga kuwaandaa askari kukabiliana na changamoto za kisasa ikiwemo uhalifu wa kidijitali.


Aliwataka askari na maafisa wa Polisi kujiepusha na rushwa na kudumisha mahusiano mazuri na wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Polisi Tanzania,Kilichopo Kidatu wilayani Kilombero SACP Zarau Mpangule alisema wahitimu hao wamepatiwa mafunzo ya sheria, uongozi, Polisi Jamii na huduma kwa wateja.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dustan Kyobya alisisitiza  nidhamu na uaminifu ni msingi wa mafanikio ya Jeshi la Polisi.








Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3