RC KIDO ASISITIZA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KAGERA
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido amesema kuwa kipaumbele chake katika uongozi wake katika mkoa wa Kagera ni suala la ulinzi na usalama mkoani hapo ili kulinda uslama wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa na Kanali Kido, baada ya kuteuliwa hivi karibuni kuongoza mkoa huo, RC Kido amesema kipaumbele chake kama maelekezo ya Mhe.Rais ni kuhakikisha anasimamia ulinzi na usalama wa mkoa wa Kagera.
"nitaendelea kushirikiana na wenzangu kuhakikisha nasimamia ulinzi na usalama wa mkoa kutokana na mkoa huu kuwa mpakani kama maelekezo niliyopewa na mhe.Rais ni kuhakikisha ulinzi na usalama wa mkoa unaimarishwa kwa maslai maana ya mkoa na nchi kwa ujumla"
Aidha mkuu hiyo wa mkoa amesema kuwa atasimamia miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika mkoa wa Kagera ili kuinua mkoa wa Kagera.
Awali aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesisitiza usimamizi wa miradi ya maendeleo ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa solo kuu Bukoba,barabara ya njia Nne , solo la machinga, ujenzi wa kituo cha mabasi kipya na tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam tawi la Kagera.
"kuna miradi ya maendeleo inaendelea kujengwa kama stendi mpya ya mabasi, stendi ya mjini Kati, soko kuu, soko la machinga, barabara ya njia nne na ujenzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam tawi la Kagera,
Hata hivyo Fatma Mwassa amesisitiza kilimo cha kahawa ili kuinua uchumi wa mwananchi moja moja na mkoa kwa ujumla kutokana na kupanda kwa bei ya kahawa sokoni.
"katika kuinua uchumi wa mkoa tulianzisha mashamba ya kahawa, tumeanzisha shamba la hekari elfu 10 kwa ajili ya kilimo cha kahawa"
Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa Karim Amri amemshukuru aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera kwa ushirikiano wake kwa chama hicho wakati wa uongozi wake"
Kanali Yahya Ramadhan Kido anakuwa mkuu wa mkoa wa Kagera wa 27 tangu nchi ipate Uhuru.


