Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI ARUSHA YAMEPONGEZWA KWA USHIRIKIANO WAO NA SERIKALI YA WILAYA YA ARUMERU.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI ARUSHA YAMEPONGEZWA KWA USHIRIKIANO WAO NA SERIKALI YA WILAYA YA ARUMERU.

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Afisa Tarafa ya Moshono Dominic Njunwa ameyapongeza Mashirika yasiyo ya Kiserikali amepongeza yaliyopo katika Halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru kwa kufanya kazi na Serikali kwa karibu.

Dominic ametoa pongezi hizo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mwinyi Ahmed Mwinyi wakati akizungumza katika ufunguzi wa kikao maalum, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake kila baada ya robo ya mwaka. 

Aidha katika kikao hicho Njunwa amepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mashirika hayo pamoja na mipango kazi yao ya mwaka 2026.

Kikao hicho pia kimepokea wasilisho kutoka kwa Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Arusha ndg. Stedvant Kileo, kufuatia maagizo ya Waziri wa Maendeleo ya Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum aliyoyatoa wakati wa ziara yake wilayani hapo juu ya ndg. Baraka Melami mkazi wa Kata ya Kimnyaki aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia na mkewe kwa kukatwa uume usiku wa Novemba 19, 2025.

Katika wasilisho hilo, wadau mbalimbali wa Mashirika hayo, wanaombwa kuona namna ya kuweza kumsaidia ndg.huyo kwa hali na mali ili kuweza kujikimu kwa namna mbalimbali ikiwemo kumjengea nyumba na mahitaji mengine.

Kufuatia taarifa hiyo, uongozi wa Halmashauri ya Arusha kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na mashirika hayo, umeunda kamati ya kuratibu jambo hilo ambapo wamekubaliana ndani ya siku saba kamati iwe imetoa mapendekezo ya namna gani maagizo hayo ya waziri yatakavyotekelezwa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3