Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
RC CPA MAKALLA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI.

RC CPA MAKALLA ASISITIZA USHIRIKIANO KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI.

 

Na Jusline Marco,Matukio Daima Media ,Arusha

Mkuu wa Mkoa CPA Amosi Makalla amesisitiza kuwa Mkoa wa Arusha utaendelea kushirikiana na Mahakama pamoja na kutatua migogoro kwa njia mbadala na kusisitiza kushirikiana na Mahakama katika utekelezaji wa hukumu zinazotolewa.

CPA Makalla ameeleza hayo Leo February 2,2026 kwenye Kilele cha Siku ya Sheria Nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha ambapo ametoa rai kwa Mawakili na Watumishi wa Mahakama kuzingatia uadilifu katika kuhudumia wananchi na kutoa elimu ya sheria kwa wananchi.


Kwa upande wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, Mhe. Frank Mahimbali amewataka Majaji, Mahakimu na Mawakili kufahamu unyeti wa nafasi zao katika maendeleo ya nchi kwa kusikiliza na kutoa maamuzi kwa haraka kwani Mahakama ya Tanzania ni nguvu ya haki, demokrasia na utawala bora.


Jaji Mahimbali amesisitiza umuhimu wa Mahakama kuwa kimbilio la wanyonge na ngao ya haki na nguzo muhimu katika utawala wa sheria, haki na uwajibikaji katika maendeleo ya Taifa.

Aidha amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla kwa ukomavu wake, kuheshimu na kuthamini mchango wa Mahakama nchini, huku akiapa kwa nafasi yake kutovumilia dharau na Kejeli kwa mahakama na kusisitiza kuwa Chombo hicho kinatakiwa kuwa chenye kuaminika, kuheshimika, chenye uadilifu na chenye mchango katika maendeleo ya Taifa.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3