Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
UHURU WA MAHAKAMA MUHIMU KWA  AMANI YA NCHI  - JAJI RWIZILE

UHURU WA MAHAKAMA MUHIMU KWA AMANI YA NCHI - JAJI RWIZILE

 

Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Media Kigoma

Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma Augustine Rwizile amesema kuwepo kwa uhuru wa Mahakama na majaji na mahakimu kufanya shughuli zao bila shinikizo ni muhimili mkubwa katika kuchochea Amani, uwekezaji na kuchochea maendeleo ya nchi.

Jaji Rwizile alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya sheria ikiwa ni kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama na kubainisha kuwa Majaji na mahakimu hawapaswi kupata shinikizo kutoka mamalaka yeyote wanapofanya maamuzi ya mashauri yanayowsilishwa mbele yao.


Jaji huyo wa mahakama kuu alisema kuwa pamoja na hilo ili uwepo uhuru wa mahakama ni  lazima mahakama kama taasisi iweze kusimamia rasilimali watu, fedha katika kupanga na kutekeleza majukumu yake.


Akizungumza katika sherehe hizo Mkuu wa wilaya Buhigwe,Kanali Michael Ngayarina aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma, Balozi Simon Sirro alisema kuwa majaji na mahakimu wanapaswa kuongozwa na ucha Mungu na busara ili kuweza kutoa maamuzi kwa kutenda haki.

Ngayarina alisema kuwa pamoja na hayo serikali imefanya kazi kubwa katika kufanya maboresho kwenye idara ya Mahakama ikiwemo miundo mbinu ya mahakama na utaratibu wa mahakama mtandao ili kuwezesha idara ya mahakama kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi na kusogeza huduma kwa wananchi.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3