Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MOROGORO YAOMBOLEZA KIFO CHA MFANYABIASHARA MAARUFU NA KIONGOZI WA ZAMANI WA TABORA, MOHAMED HOOD

MOROGORO YAOMBOLEZA KIFO CHA MFANYABIASHARA MAARUFU NA KIONGOZI WA ZAMANI WA TABORA, MOHAMED HOOD

 

Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wameingia katika majonzi kufuatia kifo cha mfanyabiashara mashuhuri na Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABORA), Bw. Mohamed Hood, aliyefariki dunia Februari 2, 2026.


Mzee Hood  (90) alijulikana sana katika sekta ya usafirishaji wa abiria, ambapo kwa miaka mingi alimiliki kampuni ya mabasi iliyokuwa ikihudumia safari za Dar es Salaam–Morogoro, Morogoro–Moshi–Arusha na mikoa mingine.


Kwa hiari yake mwenyewe, baadaye aliamua kusitisha biashara hiyo baada ya kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo nchini.

Mbali na shughuli za kibiashara, marehemu alikuwa pia mwanasiasa mkongwe, aliyewahi kuwa Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Manispaa ya Morogoro, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wananchi, ndugu na marafiki wameendelea kumuenzi kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jamii.

Mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika leo mjini Morogoro baada ya swala ya Adhuhuri.




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3