CCM KIGOMA YATOA MAAGIZO MIKOPO KWA WAJASILIAMALI
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma Jamal Tamim amesema yupo tayari kuweka mali zake dhamana ili halmashauri za mkoa Kigoma ziweze kutoa mikopo itokanayo na mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi ambavyo dhamana zao hazikidhi vigezo viweze kupata mikopo hiyo ili waweze kutekeleza mpango wa kuinua shughuli zao za kiuchumi.
Tamim alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Soko la Kwa Noti Ujiji mjini Kigoma akizindua maadhimisho ya kimkoa ya miaka 49 ya kuzaliwa CCM na kueleza kuwa ni lazima mikopo ya makundi maalum kwenye halmashauri itolewe ili kuchochea shughuli za kiuchumi za wajasiliamali wadogo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kuwepo kwa idadi kubwa ya wasichana, vijana na watu wa makundi maalum ambao wana shughuli za kiuchumi na shughuli zao zinafanyika kwa tija jambo hilo lina mchango mkubwa wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini kwa wananchi wa kipato cha chini.
Awali Meya wa maanispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid alisema kuwa ahadi ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Revocatus Chipando (Baba Levo) ya kuboresha mazingira na miundo mbinu ya soko la Kwa Noti Ujiji iko pale pale na kwamba kuna maboresha ya ramani mbunge huyo alitaka yafanyike ndiyo yamesbabisha kuchelewa kidogo kwa ahadi hiyo na kwamba ramani hiyo ikikamilika mpango utaanza kutekelezwa.



