ALLY STAR AFARIKI DUNIA, NI ALIYETAMBA NA ZUMBUKUKU, KUZIKWA KILOSA FEB 04
Mwimbaji maarufu wa taarab, Ally Hemed Star, anatarajiwa kuzikwa kesho Februari 4, 2026, nyumbani kwao Kilosa, mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taarab Tanzania (TOT), Bi Khadija Kopa, amesema safari ya mazishi itaanza saa 2:00 asubuhi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa mujibu wa Kopa, waombolezaji wote wanapaswa kukusanyika hospitalini hapo kuanzia saa 1:00 asubuhi kabla ya kuanza safari.
Amesema mazishi yatafanyika mara tu baada ya kuwasili Kilosa.
Ally Star alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa.
Enzi za uhai wake, marehemu alikuwa mmoja wa waimbaji waliotamba na nyimbo za mahadhi ya pwani, ikiwemo Zumbukuku, Natanga na Njia, zilizompa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki wa taarab.
