Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
ZAINAB MWAMWINDI AONYA WANAWAKE UWT IRINGA.

ZAINAB MWAMWINDI AONYA WANAWAKE UWT IRINGA.

 

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi (wa pili kushoto) akiwaongoza wenyeviti wa UWT wilaya kukata keki ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM  wakati wa maadhimidho ya UWT mkoa wa Iringa yaliyofanyika kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa picha na Matukio Daima Media

NA MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi amewataka viongozi wa UWT katika ngazi zote kuzingatia maadili ya uongozi kwa kujenga mahusiano bora baina yao na wananchi wanaowahudumia, akisisitiza kuwa mshikamano na heshima ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo na kuimarisha chama.


Ametoa wito huo leo wakati wa shamrashamra za kuelekea Maadhimisho ya Miaka 49 ya CCM ambapo Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umeandaa sherehe maalumu zilizohudhuriwa na wanachama kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Iringa, huku Mwamwindi akiwa mgeni rasmi wa tukio hilo.


Akizungumza na viongozi na wanachama wa UWT, Mwamwindi amesema viongozi wanapaswa kuanza kwa kujitathimini wao wenyewe kabla ya kuwaelekeza wengine akibainisha kuwa tabia na mwenendo wa kiongozi huakisiwa na wale anaowaongoza.

“Ninatakiwa nionyeshe mfano mzuri na hata hawa wenyeviti wa wilaya watanifuata mimi mama yao. Kama mimi nitakuwa wa hovyo, kauli zangu zikiwa za hovyo na nikishindwa kujenga mahusiano mazuri pengine  hata leo wasingekuwepo hapa wengetoa udhuru wangejua huyu mama anakwenda kutuaibisha kule kwa jinsi tunavyomfahamu kila mmoja angekwepa.


Ameongeza kuwa licha ya kutopokea malalamiko au mashtaka dhidi ya viongozi hao  ameona umuhimu wa kuwakumbusha wajibu wao kama viongozi wa chama na jumuiya  akisisitiza umuhimu wa unyenyekevu na kusikiliza wananchi.


“Naongea kama mama yenu, turudi katika mstari tutengeneze chama chetu  tuiheshimishe jumuiya yetu na tuwaheshimu wananchi wanaotupa nafasi tukiwafokea kwa sababu tumepata madaraka tutakuwa tunawakosea.


Aidha, Mwamwindi amewataka viongozi kuthamini nafasi walizopewa na wananchi kwa kuzitumia kwa uaminifu na kushirikiana nao katika kutatua changamoto za maendeleo.


“Kwa upande wa Waheshimiwa Madiwani mmeaminika sana na  wanawake wamekupeni nafasi kwasababu wanawaamini na sio kwa bahati mbaya ila mnaweza naomba makawajibike kwa jamii hawa ndio maBoss wetu ndio waliotupa nafasi sijapokea malalamiko kutoka kwenu ila naomba mkawajibike na huko ambako mmeaminika.


Pia amesisitiza umuhimu wa kuheshimiana katika nafasi za uongozi, akiwataka Wenyeviti na Makatibu wa Kata kuweka pembeni maslahi binafsi yanayoweza kuchochea migogoro, na badala yake kujenga umoja na mshikamano.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Iringa Mjini, Christina Makwayi, amepongeza mshikamano uliooneshwa na wanachama wa UWT kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Iringa akisema umoja huo unaonesha nguvu ya jumuiya hiyo katika chama.

“Nimefurahishwa sana na umoja huu wa ndugu zetu kutoka wilaya hizi tatu katika kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM ningependa sana kama Mwenyekiti utaridhia  siku moja madiwani wa wilaya nne wakutane hapa Iringa Mjini hata kwa tukio dogo la kukata keki ili kuwapongeza kwa kuchaguliwa na kuaminiwa kuwa madiwani wa wanawake katika halmashauri za Mkoa wa Iringa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3