MKANDARASI BUKOBA ATAKIWA KUZIBUA MITARO YA MAJI ILI KUEPUSHA MAFURIKO KWA WANANCHI
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media
Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 10 katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kampuni ya Shangdon kutoka nchini China ametakiwa kuzibua mitaro ya maji iliyoziba na kuweka njia mbadala za kupita wakati anatekeleza ujenzi huo ili kuwaepusha wananchi na mafuriko.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Jonston Mutasingwa, wakati akikagua shughuli ya umwagaji wa kifusi kwenye baraba ya mtaa wa Kasalani kata ya Bakoba, kufuatia shimo kubwa lililokuwa katika eneo hilo.
Mhandisi Mutasingwa amemtaka mkandarasi huyo wakati anatimiza majukumu yake ni vyema kuweka njia mbadara ya wananchi kupita lakini pia amaetaka kuzibuliwa kwa mitaro iliyoziba ili kuruhusu maji kupita katika njia yake bila kuvamia makazi ya watu.
nichukue nafasi hii kumuelekeza m kandarasi maeneo yote anapofanya kazi ahakikishe njia zinapitika kwa muda wote maana hilo ni wajibu na takwa la kisheria na nisisitize msimamizi kila siku kuzipitia barabara zote kilometa 10 ahakikishe anazikagua kuona kama zinapitika.
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amemtaka mkandarasi huyo ambaye pia anatekeleza mradi wa ujenzi wa kingo za mto kanoni kuhakikisha anatekeleza kwa wakati suala la usafishaji wa mto huo ili kuepukana na mafuriko yanayosababishwa na mtu huo nyakati za mvua.
pia nimtake shangdong atekeleze kwa wakati zoezi la usafishaji wa mto huu ili Kurusu maji kutiririka katika nyia yake na uwaepusha wananchi na mafuriko
Nao baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kasalani akiwemo Adela Medard amesema kuwa kujaa kuziba kwa mitaro katika eneo hilo kumekuwa kukisababisha makazi yake kuvamiwa na maji.
kwa kuziba kwa mitaro hiii kumekuwa kunaniathiri nyumba yangu inajaa mpaka imeanza kubomoka nyumba imejaa mashimbo tunaomba wasafishe hii mitaro kutuondolea hii adha
Naye Lameck Willibard ameomba kuzibuliwa kwa mitaro hiyo ili kuepukana mafuriko na kuraisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.
tunaiomba serikali itusaidie kutatua changamoto izibue mitaro hii ili sisi na vyombo vyetu vya usafiri tuwe salama.




