HALI HALISI YA BIASHARA YA MIHOGO MSIMU HUU WA MFUNGO
Na Catherin Kilwale (UoI) Matukio Daima Media.
Wafanyabiashara wa mihogo waliopo katika soko kuu la Mkoa wa Iringa wameeleza hali halisi ya biashara hiyo msimuhuu wa mfungo wa ramadhani na kwaresma,pia wamesema kuwa upatikanaji wa zao hilo ni mdogo kutokana na wahitaji ni wengi sana.
Wakizungumza na Matukio Daima Media, baadhi ya wafanyabiashara hao wameeleza kuwa msimu huu wa mfungo bei ya mihogo ipo juu, tofauti na misimu mingine.
Mfanayabiashara Ibrahim azary, alisema kupanda kwa bei ya mihogo msimu huu wa mfungo unatokana na baadhi ya miundombinu ya barabara ni mbovu kutoka kwa wakulima hadi kutufikia sokoni.
"Bei ya mihogo imekuwa juu kutokana na sisi wafanyabiashara tukifika mashambani inakozalishawa tunakutana na bei ipo juu, kutokana na hali ya hewa ya msimu huu ni mvua hupelekea upatikanaji mchacha wa zao hili".
Kwaupande wake mafanayabiashara Hadija Rajab amesema kuwa msimu huu wa mfungo wa Ramadhani na kwaresma hali ya biashara ya mihogo ipo juu kutokana na watumiaji ni wengi,pia mihogo hutumika kuanda futari kwa watu walio funga.
"Msimu huu wa mfungo tunajumua mihogo kwa bei kubwa kutokana na mfungo kwani gunia moja tunanunua kwa 150,000 ambapo msimu uliopita tulikuwa tunanunua kwa 135,000 ambayo hupelekea na sisi wauzaji kupandisha bei ya mihogo".
Huku Paulina Mligo,ambeye ni mununizi wa mihogo amesema kuwa zao hili linnapatika kwa shida sana pia bei imepanda kutokana na mfungo, watu wengi wanaitumia mihogo kwajili ya kuandaa chakula mda wa kufungua.
"Kabla ya mfungo kuanza bei ya mihogo ilikuwa ya kawaida lakini kufikia msimu wa mfungo bei ya mihogo imekuwa kubwa mbapo fungu moja unaumwa kwa 1000 ambapo sahzi fungu la elfu moja hakuna inaanzia shilingi 2000, bei hii inatu athiri sisi wanunuzi".
Hata hivyo wafanyabiashara hao wameiomba serikali iwaasaidia kuboresha miundo mbinu ya barabara kutoka vijijini kuja mjini ili kuwasaidia katika usafirishaji wa mazao kutoka kwa wakulima hadi kufika sokoni,ilikupunguza gharma kubwa ya usafirishaji na kulinda kipato chao msimu huu wa mfungo kutokana na hali iliyopo.
