Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CHANGAMOTO ZA BIASHARA MSIMU HUU WA MFUNGO

CHANGAMOTO ZA BIASHARA MSIMU HUU WA MFUNGO

Na Angelina Mbunda (UoI) MATUKIO DAIMA MEDIA 

Baadhi ya wajasiliamali wadogo wadogo Mkoani Iringa wameeleza changamoto wanazozipitia katika msimu huu wa mfungo yaani ramadhani na kwaresma, 

Wakizungumza Matukio Daima Media wajasiriamali hao wamesema kuwa Hali ya biashara kwa Sasa ni ngumu sana ukilinganisha na kipindi Cha nyuma na hii inatokana na mfungo unao endelea Sasa.

Mjasiriamali wa mgahawa alimaharufu kama mama ntilie Moten Emili amesema kuwa Hali ya biashara kwa Sasa ni ngumu sana kutokana na mfungo unaoendelea hivyo biashara inakua ngumu sana hasa mchana sababu watu wanakua hawali chakula adi jioni.

"Hali ya biashara kwa Sasa ni ngumu sana na changamoto sababu mchana kunakiwa hakuna wateja kabisa na hiyo inatokana na mfungo unaoendelea".

Mjasiriamali Abraham Kameta ambaye ni muuzaji wa  ndizi na nyanya amesema kuwa biashara kwa Sasa ni ngumu sana kutokana na watu wapo kwenye mfungo  hivyo  bidhaa zao zinaharibika kutokana na kukaa mda mrefu.

" Saizi biashara ni ngumu na inachangamoto kubwa sana Kwa sababu watu wengi wapo kwenye mfungo hawanunuhi mahitaji ya kutosha kama walivyokuwa wananunua mwanzo kwaiyo kama nyanya  huwa zinaharibika sana na sisi tunapata hasara na mtaji wetu ni mdogo sana".

Mjasiriamali Alex Malema amesema kuwa biashara saizi ni ngumu kutokana na Hali ya hewa pia kutokana na ramadhani na Kwa resma, hivyo mchana hakuna wateja kabisa lakini jioni walao kidogo

"Biashara kwa Sasa ni ngumu sana kutokana na Hali ya hewa vile vile kutokana na ramadhani na kwaresma hivyo mchana tunakaa tuu na hakuna wateja ila jioni walao kidogo wateja wanakuja kununua bidhaa kwa ajiri ya futari".

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3