Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WASIMAMIZI UCHAGUZI MDOGO KATA YA DIWANI ALIYEJIUA KWA KUNYWA MAJI YA BETRI WAFUNDWA

WASIMAMIZI UCHAGUZI MDOGO KATA YA DIWANI ALIYEJIUA KWA KUNYWA MAJI YA BETRI WAFUNDWA

 

Na Moses Ng’wat, Mbozi.


MJUMBE wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari, amewataka washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe, kufanya kazi kwa uadilifu, uzalendo na weledi.


Jaji Asina ametoa wito huo Februari 23, 2026, baada ya  kuwatembelea washiriki wa mafunzo hayo, yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Veronica katika mji wa Mlowo, Wilayani, yaliyoanza Februari 22 na yanatarajiwa kuhitimishwa Februari 24, 2026.


Akizungumza na washiriki, amewataka kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya kisheria ili kufanikisha uchaguzi huo mdogo kwa misingi ya haki na uwazi.

Amesisitiza umuhimu wa kufika vituoni mapema, kufanya maandalizi stahiki na kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unazingatia muda na taratibu zilizowekwa.

Kwa upande wake, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Zefania Msuva, amesema mafunzo hayo ya siku tatu yanshirikisha washiriki
76 na yamelenga kuwajengea uwezo watendaji hao ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki na amani.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3