Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
TAKUKURU NJOMBE WABAINI KASORO KWENYE MIRADI YA BILIONI 5

TAKUKURU NJOMBE WABAINI KASORO KWENYE MIRADI YA BILIONI 5

 


Na Gabriel Kilamlya MatukioDaimaAPP NJOMBE

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaagiza wakandarasi waliotekeleza miradi nane iliyokutwa na mapungufu yenye thamani ya shilingi bilioni tano kufanya marekebisho haraka kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa ili iwahudumie wananchi.


Akitoa taarifa ya utendaji kazi katika kipindi cha miezi mitatu cha Oktoba hadi Disemba 2025 mbele ya vyombo vya habari kaimu kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Noel Mseo amesema takukuru imeelekeza kufanyika kwa marekebisho ya miradi hiyo ya madarasa na Zahanati kwenye Halmashauri zote za mkoa wa Njombe vinginevyo hatua zaidi zitachukuliwa.


Aidha Kamanda Mseo amesema katika ukaguzi huo pia wamefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 12 zilizotakiwa kutengeneza milango katika Zahanati ya Havanga huko Kidegembye.

Kwa upande wao wakazi wa Njombe wametupia lawama mamlaka za serikali kwa kushindwa kusimamia vyema miradi hiyo hadi kukutwa na kasoro mbalimbali.

Kushindwa kuwajibika kwa baadhi ya viongozi wa umma kunasababisha kuwapo kwa mapungufu mbalimbali katika miradi jambo ambalo hatua stahiki zinapaswa kuchukuliwa.







Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3