Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 MBARONI KWA WIZI WA SOLAR ZA MRADI WA MAJI

MBARONI KWA WIZI WA SOLAR ZA MRADI WA MAJI

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Filemon Makungu.


Na Fadhili Abdallah,Kigoma



POLISI mkoani Kigoma imewakamata watu watatu  wakazi wa kijiji cha Mwamila wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wakituhumiwa kuiba vifaa vya umeme jua (Solar Panel) vilivyokuwa vikitumika kwenye mradi wa maji kwenye kijiji hicho.



Kamanda wa polisi mkoa Kigoma,Filemon Makungu  akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma  alisema kuwa  watu hao walikamatwa wakati polisi wakifanya doria na ndipo walipowakamata watu hao wakiwa na vifaa hivyo na wapoulizwa hawakuwa na majibu ya kutosheleza.


 


Kamanda Makungu alisema kuwa watuhumiwa walikamatwa na Solar Panel sita aina ya Day Loff zenye ukubwa wa watt 335 na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.


 



Katika tukio lingine Kamanda Makungu alisema kuwa polisi wakiwa doria walikamata mkazi mmoja wa Mtaa wa Katubuka Manispaa ya Kigoma Ujiji akiwa ni vifaa na mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa za wizi kutokana na kutokuwa na nyaraka za kumiliki mali hizo.


 


Bila kumtaja jina mtuhumiwa Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa katika doria hiyo Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na TV tatu ambapo kati yake mbili aina ya Mo Electronics za ukubwa wa nchii 32 na nyingine aina Volton nchi 75 na Radio moja Sabufa aina ya Sea Piano,  visimbuzi vitatu vya Azam TV  Star Time, simu tisa ikiwemo simu mbili za aina ya Teckno na nyingine saba za Google Pixel, mashuka 17 na doti saba za vitenge vya wax na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.



Mwisho.


Kamanda wa polisi mkoa Filemon Makungu (kulia) akionyesha kwa waandishi wa habari vitu mbalimbali vilivyokamatwa katika doria ya kuzuia uhalifu iliyofanywa na polisi.





Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3