MANISPAA YA BUKOBA YATAKIWA KUWEKA MSISITIZO SUALA LA USAFI WA MAZINGIARA KATIKA MJI WA BUKOBA
Na Anold Deogratias ,Matukio Daima Media Kagera
Mkuu wa wilaya ya Bukoba mkoani Kagera Erasto Siima ameutaka uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuliwekea mkazo suala uzoaji taka katika mji wa Bukoba ili kuepukana magonjwa ya mlipuko.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Bukoba, Dc.Siima amesema kuwa suala la usafi wa mazingira ni jambo muhimu sana kuzingatiwa ili kuisaidia serikali kuepukana na matumizi ya fedha nyingi kuwatibu watu kutokana na magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi usababishwa na uchafu.
"tuendelee kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yetu, na tuchukue hatua ili tuepukane na kutumia fedha nyingi kuwatibu watu kutokana na magonjwa ya mlipuko na tuendelee kushirikiana kusafisha mji wetu"
Naye mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba, Acton Rwankomezi amemtaka mkandarasi anayehusika na uzoaji wa taka katika mji wa Bukoba kuongeza siku za uzoaji wa taka katika maeneo yanayozalisha taka nyingi kama sokoni.
" unahitajika utaratibu mzuri wa uzoaji taka katika mji wetu, wanaozoa taka waongeze siku za kuzoa taka maeneo muhimu kama sokoni ambapo taka zinazaliswa kwa wingi angalau mara tatu kwa wiki, ili tuepukane na kurundikana kwa taka".
Kwa upande wake katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Bukoba mjini Shaban Mdoe amesisitiza kuwa suala uzoaji taka katika mji wa Bukoba kuchukuliwa kama huduma badala ya kuwa chanzo cha mapato ya halmashauri hali inayosababisha kuzorota kwa zoezi hilo.
"mkandarasi anataka kuzoa taka sasa tukitaka kupata kidogo kwenye hicho tutakuta shughuli ya uzoaji taka inakwamba na hivyo kusababisha changamoto kubwa katika mji wetu.
Naye mkandarasi anayezoa taka kwenye kata tatu za manispaa ya Bukoba Mohamed Nyundo amesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliwa nayo katika zoezi la uzoaji taka ni baadhi ya wananchi kutolipia ada ya taka hali inayozolotesha shughuli yao.
"changamoto kubwa inayotukabili ni baadhi ya wananchi kutolipa ada ya taka na kuelekea sisi wakati mwingine tushindwe kutimiza majukumu yetu".
Kwa miaka mitatu iliyopita manispaa ya Bukoba ilipatwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliosabishwa vifo vya watu wawili huku watu 14 wakiugua ugonjwa huo.






