MAENDELEO YA TEKNOLOJIA CHIPUKIZI YARASMISHA BUNIFU KATIKA MASOKO YA KIBIASHARA.
Na Matukio Daima Media, Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uendelezaji na Uhawilishaji wa Teknolojia (COSTECH), Dkt. Erasto Mlyuka ameeleza nafasi ya Tume hiyo katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake ya kimkakati ikiwemo kuchagiza Maendeleo endelevu na kuhamasisha matumizi ya Sayansi na Teknolojia na uratibu wa teknolojia chipukizi kufikia Dira 2050.
Dr. Mlyuka akijibu swali la washiriki wa Mkutano wa Go Green with imbeju liloratibiwa na Benki ya Biashara ya CRDB lilofanyika tarehe 12 Februari 2026, Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center- JKCC - Uliopo Jijini Dodoma.
" Bunifu zinazoratibiwa COSTECH zimeendelea kujibu suluhisho za wanachi kwa kutumia teknolojia chipukizi kuwezesha uhamasishaji wa utekelezaji wa Malengo endelevu katika maeneo saba (7) ikiwemo Nishati safi , Viwanda na Ubunifu , na lengo nambari 13 la uendelezaji wa Teknolojia zinazojibu changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi " alisisitiza Dr. Mlyuka.
Amengeza kuwa Tume ilimpokea na kuendeleza ulezi wa Bunifu ya Mitajanja za Maji 'Prepaid Water Meters' na kupitia Serikali iliwezshwa kuingiza bidhaa yake sokoni. Jitihada zote hizo ni Utekelezaji wa Teknolojia ya kijani huku akifafanua kuwa sio Teknolojia hiyo sio mpya ya biashara bali ni uwezeshaji wa kutafsiri matokeo ya kisayansi na kuendeleza Teknolojia zinazojibu suluhisho la wananchi.
Akijibu changamoto ya msukomo mdogo ya Mamlaka za Udhibiti Ubora kutoa mchango kwa kiasi kidogo katika kusaidia vijana wabunifu kufika Sokoni na kubadilisha wazo kufikia ubiasharishwaji kufikia viwnago vya Masoko ya Kimataifa. Serikali imechukua hatua za uwezeshaji wa kisera na maboresgo ya miongozo kupitia Tume hiyo.
" Kuanzishwa kwa uratibu wa Mwongozo kampuni changa 'Spin-off' katika Taasisi sita (6) za majaribio, ikiwemo Taasisi ya Teknolojia ya NM-AIST Arusha imeboresha Sera ya Hakimiliki 'IP' na kuimarisha mfumo wa mgawanyo wa Mapato kwa Wabunifu. Uimarishwaji wa mtandao wa TSICs zaidi ya 49+ umesaidia vijana kupata uwezo wa kulinda bunifu zao. Hivyo tatizo la ukosefu wa vipaji limetatuliwa kwa vijana wabunifu kuingiza bunifu zao kupitia uratibu rasmi wa kuunganisha bunifu kuingia Sokoni rasmi. " amesisitiza.
Amehitimisha, Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia yamewezesha utoaji maamuzi kuzingatia shahidi za kitafiti na utasaidia kulifikisha Taifa katika Dira ya 2050 na hatimae kufikia kiwango cha juu cha uchumi wa kati na kuwezesha sekta za kimkakati kufikia uchumi wa kidigitali.
" Serikali inajivunia kupitia COSTECH kwa kufanikiwa kuunganisha Sera, Tafiti, na Soko kwa kuhakikisha inasimamia Wadau muhimu wanasimamia ubiasharishwaji wa Matokeo-tafiti ya kisayansi yanachangia katika ongezeko la Biashara, Ajira na thamani ya kiuchumi ili kufikia uchumi wa juu wa kati na ufikiwaji wa Dira 2050. " amesisitiza.

