Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HALMASHAURI ZAHIMIZWA UKAGUZI BIDHAA ZA CHAKULA NA VIPODOZI

HALMASHAURI ZAHIMIZWA UKAGUZI BIDHAA ZA CHAKULA NA VIPODOZI


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Halmashauri za mkoa Kigoma zimetakiwa kufanya ukaguzi kwa wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara za chakula na vipodozi ili kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu ili bidhaaa wanazouza zilete madhara kwa watumiaji

Afisa Biashara wa mkoa Kigoma, Moshi Ndimuligo alisema hayo wakati wa kikao cha tathmini baina ya Maafisa wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Kanda ya Magharibi na maafisa biashara  wakaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi kutoka halmashauri za mkoa Kigoma.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho Moshi alisema kuwa tathmini inaonyesha kuwa kumekuwa na mwenendo wa kusuasua wa ukaguzi kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula na vipodozi sambamba na kutotekelezwa kikamilifu kwa usajili wa majengo yanayohusika na uzalishaji wa bidhaa za vyakula na kwamba haali hiyo ni hatari kubwa kwa afya za wananchi.


Afisa Biashara huyo alisemaa kuwa Halmashauri zzimekasimiwa kazi ya kufanya ukaguzi, usajili na ukusanyaji wa mapato ya maeneo yanayohusika na uzalishaji na biashara ya chakula na vipodozi lakini maafisa waliokabidhiwa jukumu la kusimamia kazi hiyo hawajatimiza wajibu wao kikamilifu huku kamati za halmashauri zinazohusikaa na ukaguzi huo zikiwa hazikutani kulingana na kalenda na utekelezaji wa majukumu yao.


Awali akizungumza katika mkutano huo Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Shirika la Viwango (TBS),Hamisi Seleleko aalisema kuwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mpango wa kusajili majengo yaanayohusika na uzalishaji wa bidhaa za vyakula ambapo kuanzi mwezi Julai mwaka jana hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana liliwekwa lengo la kusajili majengo 1555 lakini kwa kipindi hicho ni majengo 235 tu yalisajiliwa.


Seleleko alisema kuwa kutokana na utekelezaji huo duni kiasi asilimia 15 ya mapato ya usajili wa majengo ya nayojishughulisha na bidhaa za vyakula zilizokuanywa katika lengo la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 31.





Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3