WAZIRI NDEJEMBI ATOA AGIZO KWA PBPA
Jan 26, 2026
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Januari 26, 2026 amefanya kikao kazi na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) chenye lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha na kuendeleza utendaji wa wakala huo.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesm Mramba, Mwenyekiti wa Bodi ya PBPA, Dkt. Lutengano Mwakahesya, Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon, pamoja na Wajumbe wa Bodi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati.






