Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MWIKA KUSINI SASA YAJA KIVINGINE

MWIKA KUSINI SASA YAJA KIVINGINE


Na Gift Mongi,Moshi 

Katika kuunga mkono jitihada za serikali katika  kuleta maendeleo kwa wananchi wake wadau wa maendeleo katika kata ya Mwika Kusini jimbo la Vunjo wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kuchangishana fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika shule za msingi.

Lengo la jitihada hizo kama ilivyoelezwa na diwani wa kata hiyo John Tarimo ni kuwa wananchi hao waliona ni vyema kurekebisha miundombinu hiyo ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi kujisomea,

"Wananchi wameona ni vyema wakakarabati shule hizi za msingi ambazo nyingi ni kongwe badala ya kusubiri serikali ifanye kila jambo ambapo mambo mengine yapo chini ya uwezo wao"alisema Tarimo

Akiwa katika shule ya msingi Mawanda diwani huyo alishuhudia ukarabati ukiendelea ikiwemo uwekaji wa sakafu mpya katika vyumba vinne vya madarasa,uzimaji wa nyufa katika baadhi ya kuta sambamba na uzimaji wa matundu katika bati.

Pia upo ukarabati katika ofisi ya walimu sanjari na ujenzi wa ukuta katika moja ya baadhi ya vyumba hivyo ambao ulishaonesha dalili za kuanguka hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi pindi wawapo darasani

"Kazi hivi unavyoona ni jitihada zetu binafsi kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo waliopo nje ya kata yetu na hii iwe chache kwa wengine kuendelea kujitokeza kwani kazi ndio inaanza"alisema

Mmoja wa wakazi wa kitongoji cha Mawanda Peter Shirima alisema wameguswa kwa namna wananchi walivyoaguswa na maendeleo hayo na kuwa ni muda muafaka sasa kwa kila mwana jamii kuona umuhimu wa kujitoa kwa hali na mali.

"Maendeleo yanaanza na sisi wenyewe hivyo jambo hili ni nzuri tena ni mfano wa kuigwa na kwanini tusikimbilie maendeleo kama tunavyopenda kukimbilia katika mambo ya anasa?"alihoji

Shule ya msingi Mawanda ni miongoni mwao shule kongwe katika kata hiyo na kwa sasa inafanyiwa ukarabati katika mithili ya kuirudisha katika hadhi yake ya swali


Mwisho.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3