Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HAYA HAPA MAJUKUMU NA WAJIBU WA MBUNGE KWA WAPIGA KURA WAKE

HAYA HAPA MAJUKUMU NA WAJIBU WA MBUNGE KWA WAPIGA KURA WAKE

 


NA MATUKIO DAIMA APP

WABUNGE ni wawakilishi wa wananchi bunge hivyo ni vema  kama hivyo ndivyo ni vema kutambua yapi majukumu yao ya kibunge na yapi mahaba yao kwa wananchi. 

Mbali ya kuwa shughuli za kibunge zineanza toka siku walipoapishwa bungeni ni vema kukumbushana tena kuwa wabunge wanatokana na vyama vyao za siasa na kuna ahadi za chama , ahadi binafsi za mbunge (mahaba kwa wapiga kura) na wajibu wa mbunge kwa mujibu wa katiba. 

Hivyo mbunge lazima kutambua wajibu wako kwa wananchi kwa mujibu wa katiba ili kuitumikia vema nafasi yako na kujiweka kando na mahaba na uchama zaidi japo vyote ni muhimu ila vinaweza kuwagawa wananchi wako jimboni. 

Kama hivyo ndivyo nimelazimika kusoma Katiba ya Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 63 (hapo chini) chenye kuianisha madaraka ya wabunge nimekuwa nikijiuliza hii dhana ya watanzania kuwatarajia wabunge kuleta maendeleo katika jimbo moja moja kama huduma za kijamii kama vile shule, zahanati, barabara, maji na nyingine chimbuko lake nini.

Ikiwa wananchi wataendelea kuwapima wabunge wao kwa viwango vya manedeleo katika majimbo binafsi badala ya uwezo wa kuisimamia na kuishauri serikali.

Kwa kuwa Rais na Mawaziri ni sehemu ya Serikali ambayo wabunge wanatakiwa kuisimamia kwa mujibu wa katiba na ili kupata maendeleo binafsi jimboni wabunge hulazimika kuwapigia magoti mawaziri ambao kwa mujibu wa katiba hii wanapaswa kuwasimamia.

Hatuoni kwamba katika kila chaguzi watanzania hupoteza fursa ya kuingiza bungeni idadi kubwa ya wabunge wenye uwezo wa kuisimamia serikali na badala yake kuwaingiza bungeni wale wasio tambua wajibu wa kibunge. 

Kibaya zaidi kuwatoa bungeni wale walionyesha uwezo wa kuisimamia serikali lakini wakashindwa kuwapigia magoti mawaziri (wanaopaswa kusimamiwa) ili kupatiwa migao binafsi ya maendeleo jimboni. 

Hivyo ni vema kutambua wajibu wa mbunge kwa wananchi wake. 

(1) Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba hii kwa ajili hiyo.

(2) Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.

(3) Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza-(a) kumuuliza Waziri yeyoyote swali lo lote kuhusu mambo ya umma katika Jamhuri ya Muungano ambayo yako katika wajibu wake;(b) kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti;(c) kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au wa muda mfupi unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano, na kutunga sheria ya kusimamia utekelezaji wa mpango huo;(d) kutunga sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji kuwapo sheria;(e) kujadili na kuridhia mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3