Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HALI YA NCHI NI SHWARI LEO DISEMBA 9 -POLISI

HALI YA NCHI NI SHWARI LEO DISEMBA 9 -POLISI

 


Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu Dodoma kupitia kwa msemaji wa jeshi Hilo Kamanda Misime mchana huu imesema Hali ya nchi iko salama na shwari kabisa na vyombo vya ulinza na usalama vinaendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda  wananchi na. Mali zao waendelee kuwa watulivu na kusherehekea sikukuu ya Disemba 09, 2025 wakiwa majumbani mwao. 


Kamanda Misime amesema wananchi wapuuzie picha mjongeo zinazoendelea kusambazwa mtandaoni na kwamba ni za leo Disemba 09, 2025 kwani picha hizo ni za Oktoba 29, 30 na 31, 2025 wanazisambaza kwa Lengo la kupotosha umma ili uamini kuwa maamdamano yamefanyika jambo ambalo ni uzushi na uongo mkubwa. 


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3