VIKUNDI 63 VYA WAKULIMA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KIGOMA
Nov 14, 2026
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
VIKUNDI 63 vya wakulima vyenye jumla ya wakulima 2032 mkoani Kigoma vinatarajia kunufaika na uwagawaji wa Pampu 75 za umwagiliaji zenye thamani ya shilingi milioni 539 ambazo zinalenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kukifanya kilimo kuwa cha biashara badala ya kujikimu.
Mhandisi wa Umwagiliaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NARC), Mustang Katuta alisema kuwa wakulima 2032 wanatarajia kunufaika na pampu hizo ambapo kati yao asilimia 65 ni vijana Na kwamba ugawaji wa pampu hizo zinalenga kuondoa utegemezi wa kilimo kwa kutegemea mvua hasa wakati huu wa mabadiliko ya tabia nchi.
Mhandisi Matuta alisema kuwa mpango huo wa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia pampu hizo unategemea kulima mashamba yenye ukubwa wa Hekari 1395 ambapo pampu hizo zinalenga kuongeza uzalishaji na kutengeneza ajira kwa idadi kubwa ya vijana mkoani humo.
Akipokea pampu hizo tayari kwa kuzigawa kwa halmashauri za mkoa Kigoma Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro alisema kuwa kilimo cha umwagiliaji ndiyo msingi mkuu ambao serikali inaweza kuwa na uhakika wa kilimo na akiba ya chakula yenye malengo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa serikali imetoa fedha hizo kuhakikisha nchi inakuwa na uhakika wa chakula na ziada kwa ajili ya kufanya biashara hivyo akiwa msimamizi wa shughuli za serikali hatakubali kuona pampu hizo zinatumia kinyume na malengo na amezikabidhi kwa wakurugenzi wa halmashauri kusimamiea utekelezaji wake.
Mwisho.

