TAMISEMI YAIMARISHA MPANGO WA SHULE SALAMA NCHINI
Nov 9, 2026
Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wanaendesha mafunzo kwa wawezeshaji wa Kitaifa wa Mpango wa Shule Salama kupitia Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Mratibu wa Mpango wa Shule Salama na Usimamizi wa Usalama wa Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bi. Hilda Mgomapayo amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wawezeshaji wa Kitaifa ambao watawezesha mafunzo kwa waratibu wa Mpango wa shule salama, walimu wakuu, walimu ushauri na unasihi, wenyeviti wa bodi na maafisa maendeleo na Ustawi wa Jamii ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Mafunzo hayo yameanza tarehe 2 Novemba, 2026 na yatahitimishwa tarehe 6 Novemba, 2026 mkoani Morogoro na kufuatiwa na mafunzo ya washiriki katika mkoa wa Morogoro, Tabora, Arusha na IRINGA ambapo yatarajiwa kuanza tarehe 8 Novemba, 2026 hadi tarehe 19 Novemba, 2026.


