Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
PROF. KITILA MKUMBO ATAKA VIWANDA MIKOANI VITOE UNAFUU WA BEI KWA WANANCHI

PROF. KITILA MKUMBO ATAKA VIWANDA MIKOANI VITOE UNAFUU WA BEI KWA WANANCHI





Na Fadhili Abdallah,Kigoma


 


WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais mipango na uwekezaji Profesa kitila Mkumbo amewataka wamiliki wa viwanda katika mikoa mbalimbali nchini kuzingatia unafuu wa bei kwa wananchi kwa bidhaa zinazozalishwa na viwanda hivyo.



Waziri Mkumbo alisema hayo katika kongamano la siku moja na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa Kigoma akijibu malalamiko ya bei kubwa ya sement mkoani humo wakati sement inazalishwa mkoani humo.



Alisema kuwa haina maana kuwepo na kiwanda cha saruji,sukari au mafuta katika mkoa halafu bei za bidhaa hizo zinakuwa kubwa kuliko bidhaa zinazoingizwa na viwanda vingine mkoani humo jambo ambalo bado halitoi unafuu wala wananchi kuona umuhimu wa kiwanda hicho katika mkoa wao.


" Ni lazima uanzishaji wa viwanda mikoani ulete unafuu wa bei za bidhaa kwa wananchi, vichochee ajira lakini visaidie kuongeza mzunguko wa pesa hivyo wawekezaji lazima wazingatie hayo ili kuwafanya wananchi wajivunie uanzishwaji wa viwanda kwenye mikoa yao,"Alisema Waziri Kitila Mkumbo.



Awali Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Chipando maarufu Baba Levo alisema kuwa kiwanda cha sement kimeanzishwa mkoani humo lakini hakina unafuu wa bei kwa wananchi wa mkoa huo kwani bei zake ni kubwa zaidi ya sement inayoagizwa kutoka nje ya mkoa huo.




Akitoa ufafanuzi wa bei ya saruji inayozalishwa na kiwanda hicho,Meneja wa kiwanda hicho, ZHANG YING alisema kuwa malighafi ya kuzalishia sementi (Klinka) inayoagizwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ndiyo inayosababisha bei kuwa hivyo sambamba na kodi mbalimbali za uagizaji malighafi hizo na kodi za serikali.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3