Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MBINGA ANGELO MADUNDO ACHAGULIWA UJUMBE WA BODI YA SACCOS TANZANIA

KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM MBINGA ANGELO MADUNDO ACHAGULIWA UJUMBE WA BODI YA SACCOS TANZANIA


Na Mwandishi wetu.

 BAADHI  ya Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Mbinga Mkoani Ruvuma wamepokea kwa heshima  kuchaguliwa  Angelo Madundo  kuwa mjumbe wa Bodi Taifa Mapinduzi umoja  Saccos Tanzania.

 Akizungumza na mtandao huu  Emmanuel Mapunda ambaye ni  mjumbe wa kamati ya Elimu,Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mbinga amesema ushindi alioupata katibu wao wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya hiyo Angelo Madundo umewaletea heshima kwenye Jumuiya hiyo na kuwa mjumbe wa Bodi huyo ni mchapakazi ambaye anaubunifu.

Aidha Mapunda ametumia nafasi hiyo kuwapongeza na kuwashukuru wajumbe wa umoja Saccos Tanzania kwa kumchagua Madundo  kuwa hatawaangusha katika utendaji  kazi wake.

Kwa upande wake Angelo Madundo ameshukuru kwa nafasi hiyo na kuwa atafanya kazi waliomtuma kwa kutumia kauli mbiu ya Siasa na uchumi na kuwa Serikali imeshaweka Miundombinu mizuri ya uwezeshwaji kiuchumi kwenye jamii.

Mkutano mkuu taifa wa Mapinduzi Umoja Sacco's Tanzania, umefanyika Novemba 14  mwaka huu 2026 katika ukumbi wa NEC -CCM  Jijini Dodoma..

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3