Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WADHIBITI UBORA WA SHULE NCHINI  WATAKIWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA ELIMU

WADHIBITI UBORA WA SHULE NCHINI WATAKIWA KUIMARISHA USIMAMIZI WA ELIMU

Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule nchini, Dkt. Ephraim Simbeye, ametoa wito kwa Wathibiti Ubora wa Shule nchini kuimarisha usimamizi wa elimu kwa kuhakikisha shule zinafuata viwango, miongozo na taratibu zilizowekwa na Serikali kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.

Dkt. Simbeye ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Wathibiti Ubora wa Shule nchini.

Amesisitiza umuhimu wa wathibiti ubora kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji ili kubaini changamoto zinazokabili shule na kushauri hatua zinazofaa kuchukuliwa kwa ajili ya kuboresha utoaji wa elimu nchini.

Kuhusu suala la michango holela shuleni, Dkt. Simbeye amesisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo na taratibu za Serikali katika ukusanyaji wa michango, akibainisha kuwa usimamizi wa shule unapaswa kuzingatia sera na maelekezo yaliyowekwa ili kuepusha ukiukwaji wa taratibu na changamoto kwa wazazi na walezi.



 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3