Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
ROBO MWAKA 2026/2027 YAIKUTANISHA MALIASILI NA UTALII

ROBO MWAKA 2026/2027 YAIKUTANISHA MALIASILI NA UTALII

Dodoma

WIZARA ya Maliasili na Utalii imewakutanisha watalaam wake wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) kwa lengo la kuandaa Taarifa ya Upimaji wa Utendaji Kazi wa Wizara hiyo na taaasisi zake kwa kipindi cha Robo Mwaka (Julai hadi Septemba, 2026) kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Akizungumza katika Kikao Kazi hicho cha Robo Mwaka, jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Bure Nassibu, amesema ni cha kukamilisha taarifa ya upimaji wa utendaji wa shughuli za Uhifadhi na Utalii pamoja na kupata uelewa wa pamoja juu ya kazi za M&E.

Aidha, Bi. Nassibu amewataka wataalam hao kuhakikisha kuwa wanakitumia kikao hicho kikamilifu katika kuboresha taarifa za idara, vitengo na taasisi zao kama ilivyokusudiwa.

Wizara kupitia kitengo hicho mahsusi, inaendelea kuweka mikakati zaidi ya kuhakikisha kuwa kazi ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera, mipango na miradi ya Wizara na taasisi zake inachochea ufanisi  kwa watumishi wote katika usimamizi imara wa majukumu yake.




 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3