MIGOGORO YA ARDHI,NDOA NA UTELEKEZAJI WATOTO KUSIKILIZWA KUPITIA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA NJOMBE
Sep 18, 2026
Migogoro ya Ardhi,Ndoa na changamoto ya matunzo kwa watoto mkoani Njombe zinatajwa kushamili katika jamii hali iliyosababisha serikali kurejesha huduma ya msaada wa kisheria zitakazotolewa kwa siku tatu katika kituo cha mabasi cha zamani mjini Njombe.
Wakati wa utoaji huduma hizo kwa wananchi Wakili wa Serikali Toka wizara ya Katiba na Sheria Idara ya huduma za msaada wa kisheria Geofrey James Mwachayi anasema huduma hizo zinatolewa kwa awamu ya pili baada ya ile ya Mama samia Legal Aid ambapo licha ya kutoa huduma ya msaada wa kisheria lakini wananchi watanufaika na huduma nyingine za serikali.
Ripoti zinaonesha kuwapo kwa migogoro mingi ya ardhi ambapo Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria Njombe Njopace Geofrey Kaduma anasema wananchi wameanza kuelewa licha ya kuwapo kwa migogoro hiyo ambayo inahitaji jitihada zaidi
Wananchi mkoani Njombe akiwemo Carlos Msango wanasema huduma za msaada wa kisheria zinapaswa kusikilizwa pande zote ili kupata suluhu.
Kwa siku tatu mfululizo huduma za msaada wa kisheria zitatolewa kwa wananchi ili kupunguza kero na changamoto zinazowakabili wananchi.



