YANGA KUZINDUA WIKI YA MWANANCHI GEITA
Aug 3, 2026
Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa kesho, Jumanne Agosti 4, 2026, klabu hiyo itaanza rasmi shughuli za Wiki ya Mwananchi kwa kushiriki uzinduzi wa Uwanja wa Bukombe uliopo Ushirombo Mkoani Geita.
Kamwe amesema viongozi wa klabu pamoja na kikosi kizima cha wachezaji watakuwepo katika hafla hiyo maalum, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.
Aidha, ameongeza kuwa kikosi cha Yanga kitasafiri kupitia Kahama, ambapo mashabiki na wananchi wa eneo hilo watapata fursa ya kuiona timu yao kabla ya kuendelea na safari kuelekea Ushirombo kwa ajili ya shughuli hizo muhimu
