Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
*WAZIRI WA FEDHA ASHIRIKI MAZUNGUMZO YA WAZIRI MKUU NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA*

*WAZIRI WA FEDHA ASHIRIKI MAZUNGUMZO YA WAZIRI MKUU NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA*


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameshiriki kikao cha Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba Madelu, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika, Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, leo Agosti 28, 2026, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na kujadili maeneo muhimu ya ushirikiano yenye lengo la kuongeza fursa za maendeleo kwa wananchi.

Ushiriki wa Waziri wa Fedha katika kikao hicho unaendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia, hususan katika kuimarisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa, kuongeza uwekezaji katika miradi ya kimkakati na kuendeleza juhudi za Serikali za kujenga uchumi jumuishi na endelevu.

Benki ya Dunia imekuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa Tanzania, ikishirikiana na Serikali katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na miundombinu, elimu, afya, kilimo, uendelezaji wa sekta binafsi na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa uchumi na fedha za umma.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elija Mwandumbya, Kamisha Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje Wizara ya fedha, Bw. Patrick Pima, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. Mbayani Saruni, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.


 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3