MAONESHO YA UCHUMI PARACHICHI MARATHON YAZINDULIWA RASMI NJOMBE
Mkuu wa mkoa wa Njombe amezindua maonesho ya Uchumi Parachichi marathon yatakayokwenda kwa siku tatu na Kuwataka wananchi kuacha tabia ya kutupa parachichi zilizochini ya kiwango[Reject] kwani kuna viwanda vingi mkoani Hapa.
Akizindua maonesho hayo akiwa katika stendi ya zamani mjini Njombe Mtaka amesema kufunguliwa kwa viwanda kumefunga hoja ya parachichi mbovu na hivyo walime kwa kujiamini na kujipatia kipato.
Awali mratibu msaidizi wa Uchumi Parachichi marathon Ichikael Malisa amesema maonesho hayo mbali na kuhusisha masuala ya kimechezo lakini pia wanasisitiza suala la lishe Bora pia.
Kwa upande wao wakazi wa Njombe akiwemo Tumsifu sanga ambaye ni mjasiriamali anaye uza parachichi ndani ya soko kuu amesema tunda hilo kwa sasa linachangamoto katika soko huku Diwani wa kata ya Njombe mjini Deo Mazao Sanga na Mratibu wa Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Chrispin Kalinga kwa Niaba ya Mbunge wakikiri kuwa maonesho hayo ni fursa kubwa kwa uchumi wa wananchi.
Kilele cha maonesho hayo ni Agosti 23 siku ya Juma pili huku mkuu wa mkoa akiagiza kuandaliwa kwa nyama choma kwa siku zote za maonesho ili kutia hamasa kwa wananchi.





