Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
e-GA YAAHIDI KUENDELEA KURAHISISHA HUDUMA ZA SERIKALI KWA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI

e-GA YAAHIDI KUENDELEA KURAHISISHA HUDUMA ZA SERIKALI KWA TEKNOLOJIA YA KIDIJITALI

 




Na  Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media  Dodoma


MAMLAKA ya Serikali Mtandao (e-GA) imesema itaendelea kuendeleza na kusimamia mifumo ya kidijitali inayorahisisha utoaji wa huduma za Serikali, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuifanya Serikali ifanye kazi kwa ufanisi, uwazi na kwa kasi inayokwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia duniani.


Meneja wa Mawasiliano wa e-GA, Subira Kaswaga, amesema mamlaka hiyo imeendelea kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali za umma kutengeneza mifumo inayorahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha utendaji wa Serikali. 


Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Kaswaga amesema sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta zilizonufaika na mifumo hiyo kupitia ushirikiano kati ya e-GA na Wizara ya Kilimo katika kuanzisha mfumo wa e-Kilimo.


Amesema mfumo huo unaiwezesha Wizara ya Kilimo kupata takwimu sahihi za wakulima, kusimamia taasisi zake kwa ufanisi pamoja na kurahisisha utoaji wa vibali mbalimbali vinavyohusiana na shughuli za kilimo.


Kaswaga amesema e-GA pia imeungana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kusimamia shughuli za vyama vya ushirika, unaowapa wakulima uwezo wa kufuatilia masoko ya mazao yao, kujua yanapouzwa na kuongeza uwazi katika usimamizi wa shughuli za ushirika.


"Pamoja na kurahisisha utendaji wa vyama vya ushirika, mfumo huu unawasaidia wakulima kupata taarifa kwa wakati kuhusu mazao yao na kuimarisha uwajibikaji katika usimamizi wa ushirika," Amesema.


Aidha, amesema e-GA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Mbolea (Fertilizer Information System - FIS) unaosimamia usajili wa wazalishaji na waagizaji wa mbolea kutoka ndani na nje ya nchi, huku ukiwezesha ufuatiliaji wa bei ili kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa bei elekezi.


Ameongeza kuwa mafanikio mengine ni kuunganisha taasisi mbalimbali za Serikali kupitia mifumo ya kidijitali, hatua inayowezesha taasisi hizo kubadilishana taarifa kwa haraka na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.


Kaswaga amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Dodoma na maeneo jirani kutembelea banda la e-GA katika Maonesho ya Nanenane ili kujionea mifumo mbalimbali ya kidijitali inayotumika serikalini na kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo, pamoja na namna teknolojia inavyoendelea kuboresha utoaji wa huduma za Serikali nchi

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3