Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 CCM WAAGIZA KUFANYIKA UKARABATI WA SAKAFU BWENI LA ANNE MAKINDA SEKONDARI NJOMBE

CCM WAAGIZA KUFANYIKA UKARABATI WA SAKAFU BWENI LA ANNE MAKINDA SEKONDARI NJOMBE


NA MWANDISHI WETU.

NJOMBE.Wakati serikali kupitia mfuko wa maendeleo Tassaf ikitekeleza mradi wa bweni la Shule ya  wasichana Anne Makinda Kata ya Ihanga kwa takribani shilingi milioni 160,Chama Cha mapinduzi  CCM mkoa wa Njombe kimeelekeza kufanyika kwa marekebisho ya sakafu na maji ili kuiweka sawa shule hiyo.

‎Katika ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Kamati ya siasa mkoa ikiongozwa na katibu wa CCM mkoa Julius Peter Imeelekeza kufanyika kwa marekebisho ya baadhi ya miundombinu hususani maji ndani ya bweni Hilo ili kuwanusuru wanafunzi na magonjwa ya mlipuko.

Aidha Amemtaka mkuu wa wilaya ya Njombe kuhakikisha bweni hilo linafanyiwa marekebisho ya sakafu ambayo imeanza kufumuka miezi minne tangu kukamilika kwa ujenzi na kuanza kulitumia kwani inapaswa kuendana na hadhi ya jengo.

‎‎Awali mkuu wa wilaya ya Njombe Juma Sweda Amesema kutokana na changamoto ya mlundikano wa wanafunzi kwenye mabweni Serikali  iliamua kupeleka fedha ili kujenga bweni Hilo huku taarifa ya shule hiyo iliyosomwa na Shadrack Kiyeyeu  Makamu mkuu wa shule hiyo imeeleza kuwa Tasaf wametoa milioni 130 huku Halmashauri ikitoa takribani shilingi milioni 30 katika ujenzi wa bweni Hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa Anne Makinda Sekondari akiwemo Elvina Mhando Wamekiri kuwa Bweni Hilo limepunguza changamoto ya mlundikano huku wakiomba kutatuliwa kwa changamoto ya Maji.

Sanjari na bweni Hilo lakini pia kamati hiyo imetembelea na kukagua mabweni katika shule ya sekondari Kifanya ambayo yamekamilika na yameanza kutumika.


 


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3