WAKURUGENZI NACONGO – VURUGU ZINAKWAMISHA MIRADI
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoani Kigoma wameeleza kuwa uvunjifu wa amani katika maeneo nchini unaelezwa kuwa unachangia kwa kiasi kikubwa kuchelewesha au kusitisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.
wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoa Kigoma wakizungumza katika mkutano wa Wakurugenzi
katika mkutano wa pamoja wa Viongozi wa Masshirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma kujadili ushirikiano na namna ya kufanya kazi pamoja katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi ambapo walisema kuwa mazingira ya amani na utulivu ni msingi muhimu unaowezesha mashirika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Mmoja wa wakurugenzi hao Justine Jackson kutoka Shirika la Restless Development Tanzania alisema kuwa migogoro na vitendo vya vurugu husababisha ugumu wa kuwafikia walengwa, kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi na wakati mwingine kusababisha baadhi ya shughuli kusimamishwa kabisa.
Kwa upande waku Mratibu wa miradi wa Shirika la Care Tanzania,Gidion Donalt alieleza kuwa miradi inayohusu afya, elimu, maji, kilimo, uwezeshaji wa wanawake na vijana kiuchumi pamoja na huduma za kijamii zinahitaji hali ya Amani na utulivu katika utekelezaji wake kinyume na hivyo hali hiyo huwanyima wananchi fursa ya kunufaika na huduma na programu zinazolenga kuinua ustawi wao
Akitoa salamu katika Mkutano huo Balozi Msaidizi wa Ubalozi mdogo wa Burundi mkoani Kigoma, adabert Ninahazwe e alisema kuwa Amani ndiyo msingi wa maendele kwa serikali na mashirika katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi na kwamba Burundi ina uzoefu na hali hiyo ambayo imeathiri maendeleo na ustawi wa wananchi kwa kiasi kikubwa
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO), Jasper Makala alisema kuwa mikutano ya viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kukutana na kukaa pamoja kujadili changamoto zinazowakabili ikiwemo namna ya kutekeleza majukumu yao katika hali ya usalama na Amani ili kutimiza lengo la kuisadia jamii.






