Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
‎MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA SH. BILIONI 12.58 IKUNGI

‎MWENGE WA UHURU KUKAGUA MIRADI YA SH. BILIONI 12.58 IKUNGI

 

Na Elisante John,

MatukioDaima, Singida.

‎‎Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zimeendelea leo Jumatatu, Julai 20, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, huku zikitarajiwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 12.58.

‎Mwenge huo umeingia Ikungi ukiwa katika siku yake ya pili mkoani Singida, ukitokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, baada ya kuwasili kutoka mkoani Manyara siku ya jumapili julai 19, 2026.

Akipokea Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson Mwang'onda, amesema jumla ya miradi saba itapitiwa na Mwenge kwa kuwekewa mawe ya msingi, kuzinduliwa na kutembelewa, huku pia programu tano zikitarajiwa kukaguliwa.

"Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, Wazo Michael Mwang'onda, karibu sana Ikungi. Wananchi wa wilaya yetu tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutuwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi na kutupatia fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo," alisema Mwang'onda.

‎Kwa upande wa Mkoa wa Singida, Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zinapita katika halmashauri saba ambazo ni Singida Vijijini, Ikungi, Manyoni, Itigi, Manispaa ya Singida, Iramba na Mkalama.

‎Mbio hizo zitahitimishwa Julai 25 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, kabla ya Mwenge wa Uhuru kukabidhiwa rasmi Mkoa wa Simiyu Julai 26, 2026.

‎MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3